Tangaza Nasi

Khan asema hatomruhusu Trump kugawagawa Waingereza

Meya wa mji wa London, Sadiq Khan, amesema hatomruhusu Donald Trump kuigawa jamii za Waingereza kufuatia shambulizi la siku ya Jumamosi Juni 3. Rais wa Marekani Donald Trump alimkosoa vikali Meya huyo wa mji wa London kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Trump aaliandika kuwa Sadiq Khan alitoa sababu za uongo kwa kuwaambia wakazi wa London kwamba hakukuwa na sababu ya kuwa na wasiwasi.

Sadiq Khan amesema kuwa baadhi ya watu walionekana kuchochea mgawanyiko. Msemaji wa Ikulu ya Marekani, alikanusha rais kujipatia sifa kupitia jina la meya huyo ambaye ni muislam wa kwanza kushika wadhifa huo.

Sadiq Khan amsema akijitetea kwamba alisema kwamba watu hawakupaswa kuwa na wasiwasi baada ya kupelekwa askari wenye silaha mitaani katika jiji la London.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa Mei amekosolewa kwa kupunguza 22% ya bajeti ya polisi wakati alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kutokuwa makini kwa idara ya ujasusi pia kumewekwa mashakani. Umoja wa kitaifa uliyofuata mashambulizi ya Jumamosi usiku ulishindwa kwa shinikizo la uchaguzi ikiwa zimesalia siku tatu tu kabla ya uchaguzi wa wabunge wa mapema.

Shamblizi la mjini London Jumamosi Juni 3, lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 48 na kuwajeruhi wengine wengi.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.