Tangaza Nasi

Fainali ya NBA: Golden State Warriors waendeleza ubabe kwa Cavaliers

Timu ya kikapu ya Golden State Warriors kutoka kanda ya Magharibi imefanikiwa kushinda fainali yake ya pili ya NBA dhidi ya Cleveland Cavaliers.

Katika mchezo huo uliochezwa Jumapili hii Golden wameshinda kwa jumla ya vikapu 132 dhidi ya 113 vya Cleverland.

Kevin Durant ameendelea kuwa nyota wa fainali hizo kwa upande wa Worrios baada ya kushinda vikapu 33 huku Stephen Curry akishinda vikapu 32 na kutoa rebounds 10 na assists 11.

Ushindi huo wa Worios umemfurahisha zaidi kocha wao Steve Kerr ambaye amekuwa nje katika michezo 11 iliyopita ya timu hiyo kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Wakati huo huo Lebron James wa Cavaliers aliongoza kwa kutoa assists 14 katika fainali hiyo na kushinda pointi 29.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.