Timbulo atumia saa 48 kuaanda Mfuasi
Hit Maker wa wimbo wa Mfuasi, Timbulo amesema wimbo huo ulirekodiwa kwa siku mbili tu, sawa na saa 48.
Msanii huyo amekiambia kipindi Clouds Top 20 cha Clouds FM kuwa wimbo huo kwa mara ya kwanza ulirekodiwa kwa prodyuza Maximizer na baadaye kwa Mr T Touch kwa ajili ya mixing.
“Siku ya kwanza nilirekodi verse ya kwanza na chorus, nikanza tena verse ya pili ikabaki sehemu ndogo ya katikati kama mistari miwili mitatu hivi, halafu nilipokaa kidogo siku kadhaa nikaja kumalizia kurekodi then ikawa kama sehemu ya demo zangu,” amesema Timbulo.
Mwimbaji huyo amesema alipohamisha wimbo huo kutoka kwa Maximizer wala hakukasirika lakini kuna kipindi alifanya hivyo kwa prodyuza Sheddy Clever ikazua ugomvi mkubwa.
“Unajua sometime unapofanya kazi na prodyuza ambaye hafahamiki inapofika time unamuambia ngoma yako nataka kuitoa lakini kuna vitu tunataka tuongeze wengi wanakuwa wanaonyesha ushirikiano japo wapo wachache ambao wanalalamika,” ameongeza Timbulo.

Post a Comment