Huu ndio ujumbe wa mwisho wa Zari kwa marehemu Ivan
Baada ya Ivan Ssemwanga kufariki wiki iliyopita nchini Afrika Kusini kutokana na maradhi ya moyo na kuzikwa Jumanne hii katika makaburi ya ukoo wake yaliyopo Kayunga nchini Uganda – Zari The Bosslady ameonekana kuumizwa zaidi na kifo cha aliyekuwa mumewe.
"Zari akiwa na watoto wake katika siku ya mazishi ya Ivan Ssemwanga"
Malkia huyo wa Diamond, ameandika ujumbe kupitia mtandao wa Instagram wa kumtakia marehemu apumzike kwa amani huko alipo na pia amewashukuru wote ambao wamekuwa karibu na familia hiyo katika kipindi hiki kigumu.
“Death robbed you from us but I strongly believe you are in a better place now that you are with God. Your physical presence will be missed but you will forever be remembered,” ameandika Zari katika picha hiyo hapo chini aliyoiweka katika mtandao huo.
Post a Comment