Tangaza Nasi

Biashara ya mihadarati kuwa sugu Afrika Mashariki

 media

Wafanyakazi wawili wa chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali moja mjini Dar es Salaam nchini Tanzania wamekiri kwa polisi kuwa walipasua tumbo la raia wa Ghana aliyefariki ili kuweza kumuibia mihadarati iliopasukia tumboni mwake, baada ya kuimeza.

Katika chumba cha hoteli alikofikia, kijana huyo mfanyabisahara wa mihadarati kutoka Ghana alimeza vidonge kadhaa vya mihadarati aina ya cocaine. Kwa bahati mbaya, mmoja moja ya vidonge hivyo alivyomeza kilifunguka na kusababisha mara moja kifo chake.

Mei 20 wafanyakazi wawili wa chumba cha kuhifadhi maiti ambapo mwili wa kijana huyo ulikua ulihifadhiwa, walijaribu kupasua tumbo lake na waliweza kutoa tuvifuko 32 ambamo kulikua kulihifadhiwa cocaine kabla ya kuziuza kwa mtu mwengine. Mtu huyu aliziuza tena kwa mtu mwengine, tajiri na mfanyabiashara wa mihadarati anayejulikana kwa jina la Ally Nyundo. Watu hao na madaktari wawili wanashikiliwa na polisi mjini Dar es Salaam.

Kwa miezi kadhaa, Tanzania ilianzisha vita dhidi ya ulanguzi wa mihadarati. Mapema mwezi Mei, kiongozi wa mtandao wa kibiashara wa mihadarati, Ali Khatib haji Hassan, almaarufu Shikuba, raia wa Tanzania alikamatwa na kusafirishwa nchini Marekani kwa amri ya mahakama moja nchini Tanzania.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.