Tangaza Nasi

Upinzani nchini Rwanda wapinga udhibiti wa mitandao ya kijamii

media
Nchini Rwanda, tume ya uchaguzi hatimaye itakua ikidhibiti jumbe au taarifa za kampeni zinazorushwa kwenye mtandao na wagombea katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Agosti 4. Hatua hii imekosolewa na upinzani, ambao una hofu kwamba matumizi yake yanalenga kuzuia ukosoaji dhidi ya rais Paul Kagame.
Kuanzia tarehe 14 Julai, taarifa yoyote inayoelekea kurushwa na wagombea katika uchaguzi wa urais kwenye mitandao ya kijamii itatakiwa kuwasilishwa angalau masaa 48 kwa NEC, tume ya uchaguzi ya Rwanda kabla ya kutumiwa kwake.
 Maafisa saba wa tume hii ya uchaguguzi watachunguza taarifa hizo ili kuhakikisha haikiuki sheria yoyote, amesema Kalisa Mbanda, Mwenyekiti wa NEC.
Maafisa hao wanaweza kupendekeza marekebisho kwa wagombea, lakini taarifa au ujumbe wowote ambao hautopea idhini kutoka kwa NEC hautorushwa kwenye mitandao ya kijami.
Katika mahojiano na RFI siku ya Jumatatu Mei 29, Kalisa Mbanda alihakikisha kwamba ni kuepuka baadhi ya kaulii kama zile ambazo zinaweza kuchochea mgawanyiko.
"Lengo ni kupunguza hasara, kwa sababu sheria ya kampeni iko wazi, inasema katika uchaguzi wagombea wanapaswa kuepuka kauli, maneno, vitendo ambavyo vinaweza kusababisha raia kujihusisha na matendo ya ukosefu wa usalama na kuchochea mgawanyiko katika wananchi wa Rwanda, "alisema Kalisa Mbanda.
Hatua haijapokelewa kwa kauli moja nchini Rwanda. Mgombea aliyejitangaza kuwania katika uchaguzi wa urais, Frank Habineza, kiongozi wa chama cha Democratic Green Party, chama cha upinzani kimoja pekee kilioruhusiwa nchini Rwanda kimesema kina "wasiwasi mkubwa".
"Si haki kwa sababu tunaamini kwamba mitandao ya kijamii ni kitu kinakuja tu mara moja, amesema Frank Habineza. Tatizo jingine ni kwamba tuna hofu kwamba ujumbe muhimu kwa chama tawala unaweza kuzuiliwa na kutoa hoja kuwa ni katika hali ya kuhatarisha usalama wa taifa," ameongeza Bw Habineza.
Frank Habineza pia amehakikisha kufungua mashtaka dhidi ya tume ya uchaguzi nchini Rwanda.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.