Rais Magufuli Atoa Neno Kwa Watumishi wa Uma
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli leo wakati akizindua
Mfumo wa serikali wa ukusanyaji kodi kwa njia ya Kieletroniki amewachana
baadhi ya watumishi wake akisema wamekuwa wakiwaza mambo makubwa ambayo
wanashindwa hata kuyatimiza.
Rais
Magufuli amesema kuwa watumishi wengi wamekuwa si wabunifu katika
kuangalia vyazo vya mapato ambavyo vinaweza kusaidia serikali kuingiza
pesa nyingi lakini wao wamekuwa wakiwaza kuongeza bei ya pombe tu na
kuacha vitu vingine ambavyo vingeweza kuongeza mapato kwa serikali kwa
njia nyingine nzuri.
"Saizi
watu wanahangaika na Machinga wakati tungeweza kutengeneza vitambulisho
vya wamachinga na kila kimoja tukauza labda elfu kumi, Machinga
akinunua kitambulisho hicho anatambulika na serikali na kinaeleza kuwa
anapaswa kuwa wapi, je, ni shilingi ngapi tungezipata hapo kwa idadi wa
wamachinga waliopo nchi nzima? Lakini watu wetu wao wanawaza kuongeza
bei ya pombe tu, yaani tuna watu wa uchumi wengi lakini sijui hata
wanafikiria nini " alisema Rais Magufuli
Mbali
na hilo Rais Magufuli alisema hata tabia ya watu kukwepa kulipa kodi
inasababishwa na mipango mibovu akitolea mfano kuwekwa bei juu ya kodi
ya majengo jambo ambalo linafanya watu wengine kushindwa kulipa kodi
hiyo na serikali kupoteza mapato.
"Watu
wetu hawa hata kwenye kodi ya majengo unakuta wameweka mtu alipe
milioni mbili sasa hizo pesa wananchi wanazipata wapi? Ndiyo maana
wanakwepa kodi sababu hawana pesa hizo lakini kama wangeweka labda elfu
kumi, ishirini mpaka hamsini halafu wenye maghorofa labda laki mbili
ungeona kila mtu angekimbilia yeye mwenyewe kulipa kodi, kwa nyumba zote
zilizopo Tanzania tungepata shilingi ngapi? Lakini wameweka pesa kubwa
na hawazipati sababu watu hawalipi hawana hizo pesa" alisisitiza Rais
Magufuli
Katika
hatua ya mwisho Rais Magufuli aliyaomba makampuni ya simu nchini yawe
mfano wa kuingwa na ikiwezekana yawe ya kwanza kabisa kujiunga katika
mfumo huu mpya wa ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kieletroniki kwani
mfumo huu una manufaa kwa wawekezaji na Watanzania kwa ujumla.
Post a Comment