Mamia kwa maelfu ya watu wamiminika mitaani Caracas
Polisi wa kupambana na gahsia nchini Venezuela wametumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kuwasambaratisha maelfu ya waandamanaji wa upinzani jijini Caracas.
Waandamanaji hao wamekuwa wakiandamana kwa muda wa miezi miwili sasa kumpiga rais Nicolas Maduro, wanayemtaka ajiuzulu kwa kutumia vibaya mamlaka yake.
Maandamano haya ya hivi punde yamekuja baada ya maelfu ya wafuasi wa upinzani kuelekea katika wizara ya mambo ya nje.
Pamoja na kumtaka rais Maduro kujiuzulu, waandamanaji hao wanataka kufanyika kwa uchaguzi wa mapema na kuwaachiliwa huru kwa wanaharakati na wanasiasa wa upinzani.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu na ripoti za kiafya zinaeleza kuwa hadi sasa waandamanaji 59 wamepoteza maisha na mamia kujeruhiwa kutokana na maandamano haya.
Rais Nicolas Maduro hajaonyesha dalilili za kusikiliza matakwa ya waandamanaji hali ambayo huenda ikaendelea kuwa mbaya zaidi katika siku zijazo.
Post a Comment