JWTZ Kiama kwa matapeli wanaolaghai kutoa ajira
Meja Jenerali Harrison Masebo
Jeshi la Wananchi (JWTZ) limetoa onyo kali na tahadhari juu ya matapeli
wanaowadanganya wananchi kwamba watawapa ajira katika jeshi hilo pamoja
na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Mkuu wa Utumishi wa JWTZ, Meja Jenerali Harrison Masebo, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es salaam, amesema kumekuwa na wananchi wengi wakilalamikia utapeli huo huku akisema ajira za jeshi hilo zinapatikana kwa utaratibu maalum.
“Ofisi ya Utumishi Jeshini kuna mtu fulani ameniambia kuna ajira wewe mkubalie ila usiende kutoa chochote, njoo utupe taarifa sisi tutajua cha kufanya. Tutawahusisha wahusika na huyo mtu aliyekuahidi kukupa fomu tutamkamata. Lakini ukienda kule ukakubaliana naye na ukampa ulichompa ni fedha halafu ukakuta nafasi hujapata ukaja kwetu hujatusaidia. Kwahiyo napenda kutoa wito hao watu ni waongo ili utusaidie wakubalie lakini njoo utupe taarifa ningependa kutoa wito tushirikiane suala hili liishe,” alisema Meja Jenerali Masebo.
“Wito huu uingie akilini mwa wazazi na watoto lakini usikubali kudanganyika kiasi hicho ajira zinapatikana kwa utaratibu maalum kwa Jeshi la Ulinzi kwa Wananchi wa Tanzania na JKT. Sitasikia mtu aseme amedanganywa kama umedanganya utakuwa wewe umependa na kama hutapenda kudanganywa mkubalie njoo utueleze.”
Post a Comment