Tangaza Nasi

Diamond aelezea sifa za kutaka kujiunga WCB

Rais wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz ametaja sifa za kujiunga na lebo hiyo. Msanii huyo amesema ni lazima uwe umetoka katika maisha ya chini kabisa, yaani familia isiyojimudu kiuchumi.

Diamond amesema hawawezi kuchukua watu wanaotokea familia zinazojimudu kiuchumi [tajiri] kwa sababu ni vigumu kwa wao kupambana kwa kuwa kila kitu wanacho.

“Sifa ya kwanza WCB ni mtu aliyetoka katika hali ngumu, maisha magumu kwa sababu sisi tunajitahidi kujiajiri mwenyewe kwa wenyewe. Japo kuwa muziki wetu haujawa na riziki lakini angalau kidogo hichi  tule wote,” amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Tunaamini watu kutoka mtaani wanakuwa na talent ya kweli, wanakuwa na njaa ya kujituma na nidhamu kwa sababu wanaogopa wasije wakarudi tena katika mtaa. Lakini mtoto wa kitajiri mimi sikudanganyi wanakuwa hawana nidhamu kwa sababu wanajua sisi tuna hela, kwa hiyo yeye haogopi au kufanya kazi kwa bidii,” ameongeza.

Diamond amesisitiza ni mara kumi wakatumia nafasi walionayo kuwasadia wale walio mtaani kwa sababu wapo wengi na wanahitaji kushikwa mkono ili kesho na kesho kutwa wakazisaidie familia zao.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.