Tangaza Nasi

Kauli ya Serikali kuhusu wanaoambukiza VVU kwa makusudi

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Hamisi Kigwangalla, amesema kama kuna mtu anahisi ameshuhudia mtu anaambukiza watu Virusi Vya Ukikwi (VVU) kwa makusudi na ana mfahamu ni vyema akaenda kuripoti kwa mamlaka zinazohusika na usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa sheria

Dkt Kigwangalla ameyazungumza hayo leo Bungeni mjini Dodoma, wakati akijibu swali liliuliza serikali ina mpango gani wa kudhibiti watu wanao ambukiza Ukimwi kwa makusudi?.

“Sisi bunge hapa tukishatunga sheria tukaiweka kwamba imekuwa ni sheria sasa katika nchi hii, kuenforce kuna pande mbili zinazohusika na kuna ya tatu inayoangaliwa, kuna pande ya mlalamikaji na pande ya mlalamikiwa lakini pia na kuna pande ya wanaosikiliza mashauri, kwahiyo kama kuna mtu anahisi kwamba ameshuhudia kuna mtu anaambukiza Ukimwi kwa makusudi na ana mfahamu, ni vyema mtu huyo akaenda kuripoti kwa mamlaka ambazo zinahusika na usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa sheria,”alisema Kigwangalla.

“Baada ya kuripoti sasa pale serikali itachukua hatua, lakini kusema sisi tuanze kuwafuatilia watu wanaowaambukiza virusi vya Ukimwi watu wengine litakuwa suala gumu sana.”

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.