Licha ya uwingi wa nyota wapya msimu uliopita ila ni
wachezaji wachache pekee ndiyo walifanikiwa kufikia angalau nusu ya
matarajio
Zaidi ya milioni 500 zilitumika msimu uliopita kwenye usajili wa
wachezaji nyota kutoka sehemu mbalimbali Afrika walifanikiwa kujiunga na
Ligi Kuu Bara kwa msimu ulioisha.
Licha ya uwingi wa nyota wapya msimu uliopita ila ni wachezaji
wachache pekee ndiyo walifanikiwa kufikia angalau nusu ya matarajio.
Usajili baadhi kwa msimu uliopita ndiyo ulifanya vizuri na kurudisha thamani japo kidogo kwa klabu yake.
Goal inakuletea usajili bora kumi uliofanya vizuri msimu uliopita.
10.Stephan Kingue
Kiungo mkabaji wa Azam, Kingue amefanya vizuri sana msimu ulioisha
kwa kujaribu kumpungunzia majukumu Himid Mao, usajili huu ni bora kwa
Azam kwenye eneo la kiungo.
9.Kwasi Asante
Mlinzi kutoka Ghana anayekipiga klabu ya Mbao Fc, mlinzi huyo
amefanya kazi kubwa msimu uliopita na kuiwezesha Mbao kusalia Ligi Kuu
na kucheza fainali ya kombe la Fa.
8.Mzamiru Yasin
Kiungo mshambuliaji wa Simba, alisajiliwa kutoka Mtibwa Sugar, msimu
uliomalizika amefanikiwa kutikisa nyavu Mara nane, ni magoli mengi
kuliko kiungo yeyote Ligi Kuu msimu uliomalizika.
7.Juma Kaseja
Amejiunga na Kagera Sugar dirisha dogo akitokea Mbeya City, licha ya
Kaseja kucheza nusu msimu ila ulitosha kumfanya kuwa mmoja wa magolikipa
bora msimu uliomalizika.
6.Yusuph Ndikumana
Amesajiliwa na Mbao Fc akitokea kwao Burundi, mlinzi huyo tayari
amesha anza kuwindwa na klabu kubwa baada ya kuwa na kiwango bora kwa
kuiwezesha klabu yake kusalia Ligi Kuu na kucheza fainali ya Fa.
5.Method Mwanjali
Mlinzi wa kati wa klabu ya Simba, Mwanjale ni mmoja wa usajili bora
msimu uliopita kwa kuifanya Simba kuwa na ulinzi bora kwa kuruhusu
magoli machache.
4.Youthe Rostand
Licha ya klabu yake ya Afrika Lyon kushuka ila Mcameroon huyo
alifanya kazi yake vizuri, Simba na Yanga tayari wameanza kuulizia
huduma yake baada ya kuvutiwa na uwezo wake.
3.Yakubu Mohammed
Kwa muda mfupi ndani ya Azam, amefanikiwa kuziba pengo la Pascal Wawa
kwa zaidi ya asilimia 60, Mghana huyo ni moja ya usajili bora Msimu
uliomalizika.
2.Shiza Kichuya
Amefanikiwa kufunga magoli 15 na kutoa pasi za magoli zaidi ya 10
kwenye Ligi msimu ulioisha, tangu ajiunge na Simba akitokea Mtibwa
amefanikiwa kurudisha thamani yake klabuni.
1.Obrey Chirwa
Amejiunga na Yanga akitokea Fc Platnumz ya Zimbabwe, alianza msimu
kwa kusuasua mwanzoni mwa Msimu, Chirwa amefanikiwa kumaliza na magoli
12 na kuiwezesha timu yake kutetea taji kwa Msimu wa tatu mfululizo.
Post a Comment