Mambo magumu Jang’ombe Boys yatupwa nje michuano ya SportPesa Super Cup
TIMU
ya Jang’ombe Boys ya visiwani Zanzibar imetupwa nje ya michuano mipya
ya SportPesa Super Cup baada ya mchana wa leo kukubali kichapo cha mabao
2-0 kutoka kwa Gor Mahia ya Kenya.
Shujaa wa Gor Mahia katika mchezo wa leo alikuwa ni mshambuliaji wa Rwanda, Meddie Kagere aliyefunga mabao yote mawili.
Kagere
alifunga bao la kwanza katika dakika 64 kabla ya kuongeza bao la pili
katika dakika ya 84 baada ya George ‘Blackberry” Odhiambo kuangushwa
ndani ya boksi na beki mmoja wa Jang’ombe Boys.
Post a Comment