Mfalme wa Morocco agoma kuhudhuria mkutano wa ECOWAS
Mfalme wa Moroco ameahirisha kuhudhuria mkutano wa jumuiya ya mataifa ya Afrika magharibi huko Liberia kufuatia uwepo wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Nyatanyahu,wizara ya mambo ya kigeni imearifu.
Taifa hilo la afrika kaskazini lina matumaini ya kujiunga katika jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi ECOWAS baada ya umoja wa Afrika kuirejesha nchi hiyo ya Morroco tangu ilipojitoa miaka 33 iliyopita.
Mfalme Mohamed VI alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa ECOWAS mjini Monrovia jumamosi na jumapili ambapo nchi wanachama wanajadili ombi la Morocco kujiunga kama mwanachama kamili wa jumuiya hiyo.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo leo jumapili kama mgeni mualikwa.
Hata hivyo baadhi ya wanachama wameamua kupunguza kiwango cha uwasilishaji wa katika mkutano huo kwa sababu hawaungi mkono ukaribisho wa waziri mkuu wa israel Benjamin Netanyahu.
Post a Comment