Michuano ya kombe la mabara kuanza Jumamosi
Michuano ya kombe la Mabara
inatarajiwa kuanza kesho Jumamosi nchini Urusi ikiwa ni mwaka mmoja
kabla ya kufanyika kwa fainali za kombe la dunia ikishirikisha mataifa
nane.
Urusi ambao ndio wenyeji wa fainali za kombe la Dunia za Mwaka 2018, hawana sifa nzuri ya kutenda haki uwanjani na mara nyingi kumekuwa tabia za kibaguzi, na FIFA imedai kuwa itaweka waangalizi wa mambo ya kibaguzi viwanjani.
Wenyeji Urusi wataanza michuano hiyo kwa kuikabili New Zealand kundi A, Jumapili Ureno watachuana na Mexico huku Cameroon ikimenyana Kundi B.
Post a Comment