Tangaza Nasi

Mchezaji wa Argentina amdunga sindano mpinzani wake wa Colombia


Mchezaji wa Argentina amesababisha rabsha baada ya kukiri kwamba alitumia sindano kumdhuru mpizani wake katika mechi ya kuwania kikombe siku ya Jumapili.

Beki Federico Allende, wa klabu ya kiwango cha chini kwa michezo ya Pacifico , alijivuna kwenye mahojiano ya radio jinsi alivyotumia sindano kumdunga mara kadhaa mpizani wake wa klabu ya juu ya Estudiantes.

Allende amesema wachezaji walihitaji kuwa werevu ili kupata ushindi.

Rais wa shirikisho la soka la Pacifico Hector Moncada ameapa kumfukuza mchezaji huyo.
''Tumekasirishwa sana. Kisa hicho kimeharibu kazi nzuri ya timu . Nitamfukuza kutoka kwa klabu.'' Bw Moncada aliambia gazeti la Clarín.'

Pacifico ilishinda mechi hiyo kwa magoli 3-2 na kuibandua Estudiantes nje ya mashindano kwa uchungu mkubwa.

Wachezaji hao walikaribishwa nyumbani kama mashujaa katika mji mdogo wa magharibi wa Jenerali Alvear waliporudi kutoka Buenos Aires, pale mechi ilipochezwa.

Mandhari mazuri yalibadilika na kuwa habari mbovu.

Allende alikubali kuhojiwa na kituo cha radio cha Cordoba's Vorterix siku ya Jumanne aliposema lazima ucheze vibaya'' ili kuzishinda timu kubwa kama Estudiantes de La Plata.

Nilikuwa nikimdunga mshambuliaji wa Estudiantes na sindano , amesema beki huyo wa Pacifico.
''Tunafahamu kwamba wachezaji wa daraja la juu hawapendi kuguswa , hawapendi kupoteza wakati ama ukiwachezea vibaya. Sasa hiyo ndio ilikuwa mbinu bora ya kutumia. Soka ni ya watu werevu,'' Allende amesema.

Mtaalam wa soka kutoka Afrika Kusini,Allende alikuwa ameficha sindano mbili katika mavazi ya kuvaa miguuni . lakini sindano moja ilivunjika , wakati muamuzi wa mchezo huo alipokuwa upande mwengine , Allende alitumia sindano nyengine kumdunga mshambuliaji wa Colombia Juan Otero mara Kadhaa.

Otero alimlalamika kwa muamuzi wakati mechi hiyo ikiendelea lakini aliangulia patupu.


Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.