Serikali ya Nigeria yawatuliza nyoyo wananchi wake kuhusu afya ya Buhari
Serikali ya Nigeria inasema hakuna haja ya kuwa na
wasiwasi kuhusu afya ya rais Muhammadu Buhari anayeendelea kupata
matibabu nchini Uingereza.
Waziri wa Habari nchini Nigeria
Lai Mohammed, ametoa hakikisho hilo jijini Abuja, wakati huu raia wa
Nigeria wakiendelea kujiuliza kuhusu hali ya afya ya kiongozi wao ambaye
hajarejea nchini kwa muda wa wiki tatu sasa tangu alipokwenda nchini
Uingereza.Buhari mwenye umri wa miaka 74, kwa kipindi kirefu mwaka huu amekuwa jijini London kuonana na madakatari wake.
Mkewe Bi.Aisha Buhar aliondoka jijini Abuja wiki hii kwenda jijini London baada ya kukanusha madai kuwa mumewe alikuwa amezidiwa na ingekuwa vigumu kwake kuongoza.
Viongozi wa dini nchni Nigeria wameendelea kumwombea rais Buhari, ambaye wakati akiondoka jijini Abuja wiki tatau zilizopita, aliwaambia wananchi wa taifa hilo kuwa Madaktari wake ndio watakaoamua ni lini atarejea nyumbani.
Post a Comment