Tangaza Nasi

Uchaguzi Mkuu Uingereza wafanyika Alhamisi hii

Mamilioni ya wananchi wa Uingereza wanajiandaa kupiga kura leo alhamisi kuwachagua wabunge wapya, huku chama kitakachoshinda kikiunda serikali. kulingana na uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari vya Uingereza.

Chama cha Waziri Mkuu Theresa May kwa sasa kinaongoza kwa asilimia 41.5 huku Labour ikiwa na aslimia 40.4, kulingana na uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari vya Uingereza.

Ushindani mkubwa ni kati ya chama cha Waziri Mkuu Theresa May na kile cha Labour kinachoongozwa na Jeremy Cobin.

Ni uchaguzi unaokuja wakati huu nchi hiyo ikiendelea kukabiliana na hatari ya kushambuliwa na magaidi lakini baada ya kuanza mchakato wa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Kura za maoni nchini Uingereza kuelekea Uchaguzi Mkuu siku ya Alhamisi wiki hii zinaonesha ushindani mkali kati ya chama tawala Conservative na kile cha kile cha upinzani cha Labour.

Chama cha Waziri Mkuu Theresa May kwa sasa kinaongoza kwa asilimia 41.5 huku Labour ikiwa na aslimia 40.4.

Jumla ya wabunge 650 watachaguliwa huku takriban watu milioni 46.9 wakiwa wamejiandikisa kupiga kura.

Chama kitakachoshinda idadi kubwa ya viti bungeni kati ya 650 vinavyowaniwa, ndicho kitakachounda serikali.

Matokeo ya viti kadha yanatarajiwa kutangazwa ifikapo usiku wa manane huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa kutangazwa ifikapo Ijumaa mchana.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.