Ufaransa yataka kupelekwa kwa kikosi cha jeshi kutoka Afrika Kusini mwa Sahel
"Ufaransa imeomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusaidia kupelekwa kwa kikosi cha Afrika Magharibi mwa Afrika katika eneo la Sahel kupambana na ugaidi na biashara ya madawa ya kulevya."
Siku ya Jumanne Juni 6 Ufaransa iliwasilisha kwa
wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa rasimu ya azimio
inayoidhinisha kupelekwa kwa kikosi cha majeshi kutoka Afrika chenye
makao yake makuu nchini Mali kupambana dhidi ugaidi na uhalifu
uliokithiri.
Ufaransa ina imani kwamba azimio hili, ambalo linasaidia kisheria na kisiasa nguvu ya pamoja inayoitwa G5 Sahel litapitishwa wiki ijayo na litapelekea kuundwa kwa mazingira yenye amani kwa kuhamasisha utekelezaji wa mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2015.
Minusma, kikosi peke cha kulinda amani wa Umoja chaa Mataifa kinachofanya kazi katika mazingira ya kupambana dhidi ya ugaidi kinapaswa kusaidiwa haraka na kikosi cha pamoja kinachoitwa "G5 Sahel".
Kikosi hiki kilichopendekezwa mwezi Machi na marais wa Burkina Faso, Chad, Mali na Niger, na ambacho kitapelekwa kwa kipindi cha awali cha mwaka mmoja kitakua na askari hadi 5,000, ikiwa ni pamoja na polisi na raia wa kawaida.
Kwa mujibu wa azimio liliyoandaliwa na Paris chini ya Sura ya 7, kikosi hiki kitakua na uwezo wote wakutekeleza majukumu yake ya kupambana dhidi ya ugaidi na pia dhidi ya uhalifu uliokithiriri, biashara ya madawa ya kulevya na wahamiaji, biashara ambayo inafadhili kwa kiasi kikubwa makundi ya kijihadi katika eneo hilo.
Bado kuamua jinsi gani kikosi cha G5 Sahel kitaratibu kazi yake katika eneo la Sahel pamoja na vikosi vya Minusma, Barkhane na vikosi vya Mali.
Post a Comment