Wahamiaji 44 wapatikana wamekufa katika eneo la Agadez
Wahamiaji barani Afrika wanaendelea kukumbwa na majanga mbalimbali. Wahamiaji wasiopungua 44, ikiwa ni pamoja mtoto mmoja walikutwa wamekufa jangwani katika eneo la Agadez kaskazini mwa Niger.
Wahamiaji hawa walikuwa wakijaribu kukuingia nchini Libya. Lakini gari lao liliharibika. Taarifa hii ilitolewa na waathirika sita kutoka Ghana na Nigeria ambao waliokolewa na mtu mmoja aliyekua akiendesha gari lake, kabla ya kusafirishwa katikakatika kituo cha Dirkou. Watu wanaendelea kudumiwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).
Mkoa wa Agadez ni kitovu cha biashara ya binadamu wanaotaka kuingia Ulaya na kwa mapambano dhidi ya wafanyabiashara, serikali ya Niger ilipitisha mwaka 2015 sheria kali ambayo inakabiliana na uhalifu wao kwa adhabu ya hadi miaka 30 jela.
Majanga haya hutokea wakati huu kutokana na hali ya hewa inayojiri, Giuseppe Loprete, Mkuu wa OIM nchini Niger katika Niamey ameiambia RFI.
Giuseppe Loprete anasema kila wiki amekua akipigia simu ya wahamiaji ambao wako katika dhiki.
"Wahamiaji siku zote husafiri na hukumbwa na majanga mbalimbali. Tumekua tukipigiwa simu kusaidia wahamiaji ambao wako katika hali ya dhiki, "Giuseppe Loprete amesema.
Post a Comment