Wanaume wenye vipara katika hatari ya kuuliwa Musumbiji
Polisi nchini Musumbiji wameonya
kuwa wamaume wenye vipara huend wakalengwa kwenye mashambulizi
yanayohusiana na uchawi baada ya kuuliwa kwa wanaume wawili kama hao
mwezi uliopita.
Wanaume hao wawili wenye vipara ambapo mmoja alipatikana akiwa amekatwa kichwa na viungo vya mwili vikiwa vimetolewa, waliuliwa katika mkoa wa Zambezia.
"Mwezi uliopita mauaji ya watu wawili wenye vipara yalisababisha kukamatwa washukiwa wawili," msemaji wa polisi Inacio Dina alisema kwenyr mkutano wa waandishi wa habari mjini Maputo.
Mwandishi wa BBC mjini Maputo anasema kuwa baadhi ya watu wana imani potovu kuwa watu wenye vipara wako dhahabu kwenye vichwa vyao.
Visa vya kuuliwa watu wenye vipara kwa uchawi havijaripotiwa siku za nyuma.
Washukiwa ni vijana wa Msumbiji waliowaambia polisi kuwa viungo hivyo vingetumiwa kwa uchawi nchini Tanzania na Malawi.
Source : BBC
Post a Comment