Tangaza Nasi

Wasanii wanaokwenda kwa waganga wana tamaa – Dully Sykes


Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amefunguka na kusema wasanii au watu wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji ili kufanikiwa wanaongozwa tu na tamaa na kutoridhika na kile wanakichopata.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa yeye hawezi kufanya hivyo kwani anaridhika na maisha yake.

“Mimi maisha yangu naridhika nayo japo si makubwa kiivyo, naridhika na kagari ambacho naendesha, naridhika na mahali ninapolaza ubavu wangu, naridhika na chakula ninachopata, ninaridhika na kipato ninachopata japo ni kidogo ila nagawana na wenzangu, watoto na familia,” amesema Dully Sykes.

“Sifikirii kama kuna mganga ambaye anaweza kufanya mimi nikapata hela zaidi ya hapa, sana sana watanimaliza hela zangu,” ameongeza.

Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune!


Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.