Zitto Kabwe Apinga Gazeti la Mawio Kufungiwa

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto kabwe amepinga vikali hatua ya kufungiwa kwa gazeti la MAWIO na kudai kuwa hatua hiyo inawanyima Wananchi mawazo mbadala.
==>Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto ameandika yafuatayo;
“Uamuzi
wa kufungia gazeti la Mawio unapaswa kulaaniwa na kila mwanademokrasia.
Uhusika wa Marais wastaafu kwenye mikataba ya madini umesemwa na Rais
Magufuli Mwenyewe sio Mawio.
"Hakuna
mkataba ulioingiwa bila Baraza la Mawaziri kuidhinisha. Kitendo cha
Kamati ya Rais kutuhumu Mawaziri wa zamani mbele ya Rais Magufuli na
yeye Mwenyewe Rais Magufuli kusema hatapona mtu ilikuwa ni dhahiri kuwa
Rais anawachimba watangulizi wake.
"Kwa
sisi tuliofundishwa lugha ya Uongozi tuling’amua mapema kuwa Rais
Magufuli alikuwa anawatuhumu wenzake. Hivyo Gazeti la Mawio lilitafsiri
tu maelezo ya Rais. Kitendo cha Rais kuonya kuwa Marais wastaafu waachwe
ilikuwa ni KUJISEMESHA tu na kufungia gazeti la Mawio ni ‘ panick ‘ ya
Rais Magufuli baada ya kuwasema watangulizi wake.
"Kila wakati Rais analia kuhujumiwa na kutaka kuombewa; Adui wa Magufuli ni Magufuli mwenyewe.
"Serikali
ifungulie Gazeti la Mawio mara moja bila masharti kwani kulifungia ni
kuwanyima Watanzania mawazo mbadala kuhusu mambo ya hovyo yanayoendelea
nchini kwetu.
na kumalizia kwa hashtag ya #PressFreedom #UhuruWaHabari.”
Post a Comment