Kampuni ya uchimbaji madini ya
Acacia imekubali kuilipa serikali ya Tanzania nyongeza ya mrabaa wa kati
ya asilimia 4 mpaka 6 kama ilivyoainishwa kwenye muswada wa sheria
mpya ya madini nchini humo.
Serikali ya Tanzania na kampuni ya
Acacia ziliingia katika mgogoro mapema mwezi tatu mwaka huu kutokana na
kuzuiliwa kwa makontena 256 ya Mchanga wa dhahabu (makinikia) kwenye
bandari ya dar es salaam baada ya kubainika kuwa Acacia haitoi taarifa
sahihi ya kiwango cha madini kilichopo katika mchanga huo hivyo kulipa
tozo zisizo sahihi kwa karibu miongo miwili jambo ambalo linapingwa
vikali na kampuni hiyo.
Licha ya kukubali kulipa ongezeko hilo Acacia imesema bado inaendelea
kutathimini athari zozote zinazoweza kujitokeza kutokana na kuundwa kwa
sheria hiyo mpya.
Jiunge na BongoTune sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune
Post a Comment