Bunge la Tanzania lapitisha sheria za madini
Bunge nchini Tanzania limepitisha
sheria mbili muhimu za uchimbani madini ambazo zina lengo la kuleta
mabadiliko makubwa katika sekta ya madini.
Kupitia sheria hizo sasa serikali ina matumaini kuwa wananchi watanufaika kutokana na mali asili ya nchi hiyo.
Moja ya sheria hizo inasema kuwa watu nchini Tanzania watakuwa na uhusu wa kudumu kwa mali yao ya asili na serikal kwa niaba ya watu itasimamia mali hiyo.
Hadi sasa sheria haikuweza kueleza wasi ni nani ana uhuru wa kusimamia mali asili ya nchi ya Tanzania.
Sheria nyingine inaipa bunge mamlaka ya kutathmini makubaliano yanayofanywa na serikali kuhusu mali asili.
Serikali inalaumu kampuni ya Acacia kwa kutofichua kiwango cha madini inachopeleka nje ya nchi na kukosa kulipa kodi ya mamilioni ya dola kwa muda wa miaka 20 imekuwa ikihudumu nchini humo.
Kampuni hiyo hata hivyo imepinga takwimu hizo za serikali ikisema kuwa ikiwa zilikuwa za ukweli basi Tanzania ingekuwa mzalishaji mkubwa zaidi wa dhahabu na shaba duniani.
SOURCE BBC


Post a Comment