Hatma ya wanariadha wa kike wenye homoni nyingi za kiume kujulikana
Utafiti mpya unasema kuwa wanawake
wanaozaliwa na viwango vya juu vya homini za kiume {Testosterone} wana
uwezo mkubwa wa utendaji ikilinganishwa na wenzao katika mashindano.
Imechapishwa wiki chache kabla ya mahakama ya usuluhishi kuhusu maswala ya michezo kutoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu uamuzi wa shirikisho la wanariadha duniani I.A.A.F kuwapiga marufuku wanariadha wa kike walio na homoni nyingi za testosterone.
Marufuku hiyo ilioanzishwa 2011,ilisitishwa na mahakama hiyo miaka miwili iliopita.
Watafiti wake wanasema kuwa ushirikiano kati ya viwango vya juu vya homini za testosterone na utendaji bora haufai kuchukuliwa kama thibitisho.


Post a Comment