Moto wateketeza soko kubwa zaidi nchini Zambia
Nchini Zambia soko kubwa zaidi nchini humo limeteketea moto.Soko hilo la City Market lililo mjini Lusaka, limekuwa likiteketea tangu mapema leo na limeteketeza badhaa nyingi zilizo kuwa katika soko hilo.
Walioshuhudia wanashuku kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme na kuwalaumu wazima moto kwa kuchelewa kufika kuzuia moto huo kusambaa.
Mamlaka nchini humo bado zinachunguza chazo cha moto huo uliosababisha hasra kubwa kwa wafanya biashara wanaotumia soko hilo.
Soko hilo lina wafanyabiashara wengi zaidi nchini Zambia. Kati ya bidhaa zinazouuzwa ni pomoja na nguo za mitumba, vifaa vya elektroniki na hata chakula.


Post a Comment