Korea Kusini yataka mazungumzo ya kijeshi na Korea Kaskazini
Korea Kusini imependekeza kufanyika
mazungumzo ya kijeshi na Korea Kaskazini, baada ya majuma kadhaa ya
msukosuko, kufuatia hatua ya Korea Kaskazini ya kufanya majaribio ya
makombora.
Ikiwa mazungumzo hayo yatafanyika, yatakuwa ndiyo ya kwanza ya juu tangu mwaka 2015.
Maafisa wa vyeo vya juu walisema kuwa mazungumzo hayo yatalenga
kisitisha vitendo vyote vyote ambavyo huchangia kuwepo misikusuko ya
kijeshi katika eneo lenye ulinzi mkali kati ya Kusini Kaskazini.
Rais
wa Korea Kusini Moon Jae-in tangu mwanzo alikuwa ameashiria kuchukua
hatua ya kuleta ushirikiano wa karibu na Korea Kaskazini.
Akitoa hotuba hivi majuzi mjini Berlin, alisema kuwa mazungumzo na
Korea Kaskazini yanastahili kufanyika na kutaka muafaka kuafikiwa.
Lakini
hatua za Korea Kaskazini kuyafanyia majaribio makombora likiwemo la
hivi majuzi la masafa marefu, yanaenda kinyume na maazimio ya Umoja wa
Mataifa.
Naibu waziri wa ulinzi nchini Korea Kusini Suh Choo-suk, aliuambia
mkutano wa wanahabari kuwa mazungumzo yatafanyika eneo la Tongilgak,
katika jengo la Korea Kaskazini katika eneo lisilo na ulinzi mkali kati
ya nchi hizo mbili.


Post a Comment