Haji Manara atolewa kifungoni
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imemuachia huru Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Sports
Club, Haji Sunday Manara na sasa kuendelea na majukumu yake.
Manara alifungiwa kwa kutojihusisha na mchezo wa soka kwa muda wa miezi
12 na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni tisa kwa utovu wa
nidhamu wa kutoa matamshi yasiyo na stahiki kwa viongozi wa TFF pamoja
na vyombo vya uongozi wa mchezo huo.


Post a Comment