Mesut Ozil: Nataka kubaki Arsenal
Wakati akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake kuichezea timu ya Arsenal kiungo mjerumani Mesut Ozil amesema anataka kubaki katika klabu hiyo.
Swali kubwa limekuwa ni iwapo Ozil atasaini mkataba mpya au ataondoka katika klabu hiyo lakini sasa mchezaji huyo ameweka wazi kutaka kubaki katika kikosi cha Arsene Wenger.
”Ningependa kubaki katika klabu hii, kwa sasa kitu cha muhimu ni maandalizi ya timu kuelekea msimu ujao lakini tutakapo rudi Landani tutakaa na kuzungumza kuhusu hatima yangu” alisema Ozil.
Ozil alisajiliwa na Arsenal mwaka 2013 kwa kiasi cha paundi milioni 42.5 kutoka katika klabu ya Real Madrid na kuwa mchezaji aliyenunuliwa na klabu hiyo kwa kiasi kikubwa cha pesa.
Mchezaji huyo amezungumza kuhusu Alexis Sanchez anyehusishwa na mpango wa kuihama Arsenal akimtaka kubaki katika klabu hiyo.


Post a Comment