Trump na Putin walifanya kikao cha siri G20
Rais wa Marekani Donald Trump
alikutana na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin katika mkutano wa pili wa
siri ambao haukutajwa ulipofanyika katika kikao cha mkutano wa mataifa
ya G20, imebainika.
Walifanya mazungumzo baada ya mkutano wao wa kwanza lakini ukulu ya White House haijatoa maelezo kuhusu kile kilichozungumziwa.
Rais Trump amekana madai ya kufanyika kwa mkutano huo wa siri na Putin na kusema ni ''habari bandia''.
Wapelelezi wa Urusi wanaamini kwamba Urusi ilimsaidia bwana Trump kushinda uchaguzi wa mwaka jana kitu ambacho Urusi imekana.
Bwana Trump amepinga madai kama hayo.
Mkutano wa pili ulifanyika wakati wa chakula cha jioni cha viongozi katika kikao hicho cha G20 mjini Hamburg mapema mwezi huu
Rais wa Marekani alikuwa pekee na Putin alikuwa na mkalimani wake huku vyombo vya habari vya Marekani vikisema kuwa mkutano huo ulichukua saa moja.
Madai ya kilichozungumzwa yaliwasilishwa kwa maafisa wa Ikulu ya Whitehouse na bwana Trump mwenyewe kwa kuwa hakukuwa na wasaidizi wakati wa mkutano huo.


Post a Comment