Wanajeshi 34 wa Cameroon hawajulikani waliko baada ya meli yao kuzama
Wanajeshi 34 wa Cameroon bado hawajapatikana, siku
moja baada ya meli yao kuzama katika Pwani ya nchi hiyo mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Ripoti zinasema kuwa, meli hiyo ilikuwa na abiria 37 ikielekea katika mji wa Bakassi.
Waziri wa Ulinzi Joseph Beti Assomo amesema wanajeshi watatu ndio waliokolewa wakiwa hai baada ya kuzama kwa meli hiyo.
“Wanajeshi 34 bado hawajukani waliko lakini watatu wameokolewa,” amesema Waziri Assomo.
Meli hiyo ilikuwa imewabeba wanajeshi wa nchi hiyo wanaoaminiwa
kupambana na kundi la Boko Haram kutoka nchini Nigeria Kaskazini mwa
nchi hiyo.
Wizara ya ulinzi nchini Cameroon imesema meli hiyo ilipoteza
mawasiliano kuanzia mapema wakati ikitokea jijini Duala ikielekea Bakasi
saa moja kabla ya kupoteza mawasiliano.

Post a Comment