Majibu ya Jux alipoulizwa kama anaweza kujiunga WCB
Msanii wa Bongo Flava, Jux amesema anaweza kujiunga na record label
yoyote endapo watafikia makubaliano ila sio kitu ambacho amekifikiria
kwa sasa.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya
‘Utaniua’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio Wasafi record ni label
nzuri ila hajawahi kuongea kitu kama hicho.
“Ni kitu kizuri sio kibaya kwa sababu ile ni record label, hiyo
nafasi ikipatika sio mbaya lakini kwa mimi sikuwahi kufikiria kwa hapa
Tanzania au kwa Africa kwa kweli,” amesema.
“Iwe ni kampuni au sehemu ambayo itanichukua mimi kama kunimeneji
pale nilipokuwa wafanye vitu extra zaidi. Sawa wanaweza ikawa wanaweza
kwa mkataba kama watakuja na mkataba ambao nitautaka na vitu vyangu
ambavyo navihitaji naweza nikasaini kwa sababu mimi ni mfanyabiashara
lakini kwa sasa hivi hatukuwahi kuongea au kufikiria,” ameongeza.


Post a Comment