AU: Uhuru na Raila hawakubaliani juu ya utayarishaji wa uchaguzi
Umoja wa Afrika unasema rais Uhuru Kenyatta na Mgombea mkuu wa upinzani Raila Odinga wanatofautiana kuhusu maandalizi na utayari wa Tume ya Uchaguzi kusimamia Uchaguzi Mkuu mwezi ujao.
Hili limebainika baada ya
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja huo Moussa Faki Mahamat kumaliza ziara yake
nchini humo baada ya kukutana na viongozi hao wawili, mashirika ya
kiraia na Tume ya Uchaguzi.
Odinga amekuwa akihoji utayari wa tume ya Uchaguzi, huku rais
Kenyatta akisisitiz akwua ni lazima Uchaguzi ufanyike tarehe nane mwezi
ujao na kuwashtumu wapinzani kutaka uchaguzi huo kuahirishwa.
Kiongozi wa waangalizi wa Umoja wa Afrika ambaye ni rais wa zamani wa
Afrika Kusini Thambo Mbeki amesema wamekutana na wadau mbalimbali
kuhakikisha kuwa maandalizi yanakuwa mazuri.
Siku ya Alhamisi Mahakama ya rufaa iliamua kuwa tume ya Uchaguzi
inaweza kuendelea kuchapisha karatasi za kuwania urais . Haijabainika
ikiwa upinznai utakataa rufaa katika Mahakama ya juu.


Post a Comment