Vijana 6 kutoka Burundi watoweka Marekani
Taarifa kutoka vyombo vya usalama nchini Marekani zinabaini kwamba vijana sita kutoka Burundi waliokuwa wakishiriki katika mashindano ya roboti nchini Marekani wametoweka, na haijulikani walipo, taarifa ambayo haijathibitishwa na serikali ya Burundi.
Waandalizi wa mashindano hayo
wanasema kuwa waliwaeleza polisi baada ya msimamizi wa timu hiyo ya
Burundi kushindwa kuwapata vijana hao.
Idara ya polisi mjini humo imesema kuwa mara ya mwisho vijana hao
kuonekana ilikuwa siku ya Jumanne wakati wa makamilisho ya michezo hiyo.
Vijana hao ambao ni wavulana wanne na wasichana 2 walio kati ya umri
wa miaka 16 na 18 walipotea wakati wa mashindano hayo ya kwanza duniani
yaliofanyika Washington DC.
Vijana hao wanatambulika kuwa Don Ingabire, Kevin Sambukiza, Nice
Munezero, Audry Mwamikazi, Richard Irakoze na Aristide Irambona.
Kulingana na gazeti la The Washington Post, msemaji wa mashindano
hayo Jose Escotto alisema, ripoti kamili imewasilishwa kwa polisi ambao
wanachunguza kisa hicho.
Mashindano hayo yyaliyohudhuriwa na timu 150 yanalenga kuwashawishi
vijana kukuza vipaji vyao katika masomo ya sayansi, technolojia,
uhandisi na hesabu.
Taarifa zaidi kutoka yombo vya usalama zinasema kuwa vijana wawili kati yao tayari wamevuka mpaka na kuingia nchini Canada.
Idara ya polisi ilibandika picha za sura za vijana hao sita waliopotea katika mtandao wao wa Twitter.
Polisi imewataka raia kuwasiliana nao iwapo watakuwa na habari yoyote kuhusu vijana hao.

Post a Comment