Aveva hali ya Afya siyo nzuri alazwa ICU
Kesi ya madai ya utakatishaji fedha inayomkabili Rais wa klabu ya
Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, imesomwa leo
na kupelekwa mbele mpaka tarehe 22, machi 2018.
Kutokana na Evans Aveva ambaye ameripotiwa kuwa amelazwa katika
kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH), hali iliyopelekea kushindwa kuhudhuria mahakamani kusikiliza kesi
hiyo inayomkabili.
Hayo yameelezwa leo Machi 8, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard
Mashauri na wakili anayewatetea, Evodius Mtawala wakati kesi hiyo
ilipotajwa mahakamani hapo.
”Mshatakiwa wa Kwanza Aveva tangu jana amelazwa katika kitengo cha
wagonjwa mahututi hali yake siyo nzuri” amesema Wakili Mtawala.
Hata hivyo mwendesha mashataka wa Takukuru Leonard Swai naye
ameliambia mahakama kuwa Aveva ni mgonjwa na kwamba upelelezi wa kesi
hiyo bado haujakamilika.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Mtawala ameiambia mahakama kuwa
walizungumza na upande wa mashtaka wataeleza jalada la kesi hiyo bado
lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), na wameomba wapewe siku 14 ili
waweze kueleza kiti.
Kwa mara ya kwanza Kesi hiyo ya madai ilitajwa Julai 20, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu
ya Simba na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na
wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka 2017.

Post a Comment