Nondo apatikana akiwa hai Mafinga
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania , Abdul Nondo
ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam aliye ripotiwa
kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la
Mafinga mkoani Iringa.
Inadaiwa kuwa alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka
usingizini na kuwauliza wenyeji wa eneo alilo jikuta kuwa yuko wapi,
ambapo walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha
akapelekwa kituo cha polisi.
Aidha, Abdul Nondo alionekana kwa mara ya mwisho Jumanne katika Ofisi
za Tahliso jijini Dar es salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu
taarifa iliyokuwa imetolewa na Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu
nchini Tanzania.
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) ulisema baada ya kuondoka Ofisi
hizo, Nondo alielekea chuoni na kuaga kuwa anaondoka kwenda nyumbani
Madale.
Hata hivyo, kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo alielezea kuwa
alikuwa akifuatiliwa mara kadhaa na watu wasiojulikana wakijitambulisha
kama watu wa usalama ambao wamekuwa wakimpatia vitisho.

Post a Comment