Tangaza Nasi

Tetesi: Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri kurithi mikoba ya Conte Chelsea


Klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza huwenda ikamsajili kocha wa timu ya Juventus, Massimiliano Allegri na kurithi mikoba ya Antonio Conte anayetarajiwa kufungashiwa virago mwishoni mwa msimu.

Allegri huwenda akatua Stamford Bridge mwishoni mwa msimu lakini kama itashindikana mazungumzo na meneja wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique hii ni kwamujibu wa chombo cha habari cha Star
Kufuatia matokeo mabovu wanayopata Chelsea ikiwa chini ya Conte hasa kipigo cha nyumbani cha mabao 3 – 1 dhidi ya Toottenham ikiwa ni mara ya kwanza kutokea Stamford Bridge tangu mwaka 1990 kimezidi kumuweka kwenye hali mbaya zaidi.
Allegri alishawahi kuhusishwa na kujiunga na Arsenal kuziba nafasi ya Arsene Wenger lakini kwa sasa amekuwa akihushishwa zaidi na Chelsea.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.