Manara ameonesha jezi za kupokelea Ubingwa Simba SC
Club ya wekundu wa Msimbazi Simba SC Jumamposi ya May 19 2018 uwanja wa Taifa Dar es Salaam itakabidhiwa Kombe lao la Ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom msimu wa 2017/2018.
Taarifa rasmi zilizotoka kutoka kwa afisa habari wa Simba ni kuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli ndio atakuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo ya kuikabidhi Simba taji.
Pamoja na kuwa TFF na bodi ya Ligi kukubali kushusha viingilio vya mchezo huo kutokana umaalum wa mchezo wenyewe, afisa habari wa Simba Haji Manaraameonesha jezi ambazo mashabiki ameomba wazinunue wakashangilie nazo Ubingwa uwanja wa Taifa.
Post a Comment