Mtoto mchanga aokotwa akiwa amefariki
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa Mtendaji wa Mtaa huo, Majolino Myinga amesema kuwa alipigiwa simu na wananchi wa mtaani hapo baada ya kuona mtoto mwenye jinsia ya kike akiwa amekufa baada ya kutupwa na mtu asiyejulikana katika mtaa huo.
“Tumejaribu kuangalia mtoto huyo tumekuta ameshakufa lakini aliyetupa bado hajulikani tumepeleka taarifa polisi kwa ajili ya kufanya uchunguzi ili waweze kubaini aliyefanya ufanyama huo.” Amesema Myinga
Aidha Afisa huyo amesema kuwa matukio hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika mtaa huyo ambapo hadi sasa tukio hilo ni la nne la watu wasiyojulikana kutupa watoto katika mtaa hapo.
“Wito wangu kwa jamii kuacha tabia hizi za kinyama ambazo hazikubaliki ndani ya jamii kama mtu anaona mwanaume ambaye amempatia ujauzito huo lakini anashindwa kumsaidia ni bora atoe taarifa katika ofisi za Serikali kwa sababu hali hii haitupendezi hata kidogo.” Amesema Afisa huyo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo, Mernkon Ndelwa amesema tangu mwaka jana matukio hayo yameanza kujitokeza akina mama kutupa watoto wachanga lakini hadi sasa bado hawafahamiki wanatoka katika maeneo gani.
” Hali hii inasababishwa na mwingiliano wa watu kutoka sehemu mbalimbali lakini tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kuwapata wahusika wa matukio hayo ili sheria iweze kushika mkondo wake.” Amesema Ndelwa
Naye mmoja wa shuhuda wa tukio hilo, Farida Salum amesema kuwa wanawake wengi wanashindwa kujitambua hali ambayo inapelekea kutokea kwa matukio hayo.
“Hii ni Dhambi kubwa ambayo wanawake tunaifanya haiwezekani anakubali kubebe mimba ya miezi tisa alafu anajifungua mtoto kisha anamtupa hali hii haipendezi hata kidogo.” Amefafanua Salum
Chanzo mwananchi.
Post a Comment