Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 17.03.2022
Mshauri wa Borussia Dortmund Matthias Sammer amegusia kwamba mshambuliaji Mnorway wa timu hiyo Erling Braut Haaland, 21 ataondoka katika klabu hiyo ya Ujerumani kujiunga na Manchester City. (Amazon Prime, via Goal)Haaland anahusishwa pia Real Madrid lakini anapaswa kupunguza mshahara wake kama atataka kujiunga na klabu hiyo ya Hispania. (Marca)Vilabu vinavyomtaka Haaland vitapaswa kukubaliana na kipengele katika mkataba wake - ambacho kinaaminika ni kulipa £63m - mwishoni mwa April. (Bild, via 90 Min)
Paris St-Germain imewasiliana na meneja wa Tottenham Antonio Conte, ambaye ana kipengele katika mkataba wake wa sasa kinachomruhusu kuondoka Spurs mwishoni mwa msimu. (Calciomercato, via Football Italia) Meneja wa Arsenal Mikel Arteta yuko katika orodha ya majina ya makocha wanaowaniwa na PSG kumrithi meneja Mauricio Pochettino, lakini mhispania huyo anasema "ana furaha sana" pale kwa washika bunduki hao wa London. (Mirror)Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi hana mpango wa kutimka PSG, ingawa nyota huyo mwenye miaka 34 amekuwa akihusishwa na klabu yake ya zamani Barcelona, hakuna mawasiliano na klabu hiyo ya Hispania. (Mail)
Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel na bosi wa Sevilla Julen Lopetegui ni miongoni mwa makocha wanaowaniwa na Manchester United wakati huu klabu hiyo inasaka meneja mpya. (Guardian)Tuchel amempiku kocha wa PSG Pochettino na kuwa chagua la kwanza la Manchester United kuwa meneja mpya na klabu hiyo ya Old Trafford na ingependa kumteua mjerumani huyo kabla msimu kumalizika. (Star)Chaguo la kiungo wa Uholanzi Georginio Wijnaldum itakua ni kurejea ligi juu ya England kama nyota huyo mwenye miaka 31 hayuko kwenye mipango ya muda mrefu ya PSG. (Teamtalk)Wakala wa Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski anasema hakuna mazunguzo yaliyofanyika kuhusu kuongeza mkataba mpya kusalia kwenye klabu hiyo ya Ujerumani. (Kicker, via 90 Min)
Post a Comment