Tangaza Nasi

Wezi wavamia nyumbani kwa Pogba akiwa uwanjani

 


Kiungo wa klabu ya Manchester United Paul Pogba ametangaza kuwa nyumba yake ilivamiwa na wezi siku ya Jumanne usiku wakati timu yake ikicheza na Atletico Madrid. Wakati huo watoto wake walikuwemo ndani wamelala.

Tukio hilo lilitokea wakati mechi inakaribia kuisha, Pogba na mkewe waliharakisha kuwahi nyumbani wakiwa na wasiwasi mkubwa.

Akizungumza kwa hisia kubwa nyota huyo amesema “nitatoa zawadi kwa mtu yeyote atakayenisaidia kupata taarifa zaidi juu ya tukio hili”.

Itakumbukwa kuwa mwezi Januari mwaka huu nyumba ya mlinzi wa Man United Victor Lindelof ilivamiwa wakati yeye na timu yake wakicheza mechi dhidi ya Brentford.

Man United imesema kuwa inafanya kazi kwa karibu na wachezaji wake ili kuimarisha ulinzi majumbani mwao.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.