Tangaza Nasi

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 31.03.2022

 

Manchester United wako tayari kumnunua mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 24, ambaye amefunga mabao 23 katika klabu ya Roma ya Italia msimu huu. (Corriere dello Sport -In Italian)

Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 26, anaweza kutumiwa na Manchester United kama suluhu katika mpango wa kumsaini nahodha wa Uingereza Harry Kane, 28, kutoka Tottenham. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 26, ameiambia Leeds United kuwa anataka kusaini mkataba mpya msimu huu, ambao unaweza kuwakatisha tamaa Manchester United, Liverpool, Newcastle, West Ham na Aston Villa . (Mirror)

Everton italazimika kumuuza mmoja wa washambuliaji wake nyota, mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 25, au mchezaji wa kimataifa wa Brazil Richarlison, 24, msimu wa joto baada ya kupata hasara ya £121m msimu uliopita.(Sun)

Manchester United wanatamani kumnunua mshambuliaji wa Benfica mwenye thamani ya pauni milioni 60 Darwin Nunez, lakini matumaini yao ya kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay yanategemea kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (Telegraph - usajili unahitajika)

Newcastle United wako tayari kumnunua beki wa Bologna na Scotland Aaron Hickey, 19, ambaye anaweza kuruhusiwa kuondoka klabu hiyo ya Italia kwa kati ya £15-£20m. (Fabrizio Romano)


Winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, 24, amedokeza kwamba yuko tayari kumaliza muda wake Tottenham msimu huu wa joto. (Mail)

Mshambuliaji wa Jamhuri ya Czech mwenye umri wa miaka 26- Patrik Schick, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda Arsenal au Barcelona, hataondoka Bayer Leverkusen, anasema Afisa Mkuu mtendaji wa klabu hiyo. (Goal)

Kiungo wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 31, alipuuza ombi la la Januari kutoka kwa Paris St-Germain la kujiunga nao msimu huu wa joto. (Le Parisien)

AC Milan wanatafakari uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio baada ya kurudi nyuma kutokana na masharti ya mshahara wa kiungo huyo wa kimataifa wa Uhispania wa miaka 26. (Tuttosport)


 

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.