Tangaza Nasi

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu tarehe 13.06.2022

 

Juventus wana uhakika na matumaimi makubwa ya kumsajili Paul Pogba, 29 bure kutoka Manchester United. Kiungo huyo mfaransa amekubali kusaini mkataba wa miaka minne. (Fabrizio Romano, Twitter)

Nyota wa Tottenham Steven Bergwijn anasema anasakwa na vilabu kadhaa wakati huu ambapo winga huyo wa Uholanzi, 24, akitaka kutimka, Ajax wako kwenye mazungumzo kwa ajili ua kumsajili msimu huu. (90min)

Kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 30, ameamua kutafuta changamoto mpya na anajiandaa kutimka Brentford. Vilabu vya TottenhamHotspur na Manchester United vinammendea nyota huyo. (Express)

Manchester United wanamfukuzia pia winga wa Brazil Antony, 22, kutoka Ajax, na kiungo wa Uholanzo Frenkie de Jong, 25, kutoka Barcelona. (Talksport)

Chelsea wanakaribia kumnasa kipa Mmarekani Gabriel Slonina, 18, kutoka Chicago Fire baada ofa ya Real Madrid ya £8.5m kukataliwa. (Fabrizio Romano, Twitter)

Leeds United wanaongoza katika mbio za kumsaka mshambuliaji wa New York City mwenye miaka 23 muargentina Valentin Castellanos. (Give Me Sport)

Kiungo Matteo Guendouzi anatarajia mlinzi William Saliba, 21, atafuata nyayo zake na kurejea Marseille kutoka Arsenal msimu huu baada ya wote kuwa kwa mkopo kwenye klabu hiyo ya Ufaransa msimu uluomalizika. (90min)

Kama mlinzi wa Ufaransa Jules Kounde, 23, ataondoka Sevilla na kujiunga na Chelsea, basi Barcelona itaelekeza nguvu zake kumsajili Kalidou Koulibaly, ingawa Napoli inaweza kutaka angalau £34.1m kwa ajili ya mlinzi huyo Msenegal. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Inter Milan inajiandaa kumsajili Paulo Dybala bure kutoka Juventus, huku mshambuliaji huyo muargentina mwenye miaka 28, anasaini mkataba wa miaka 3. (Goal)

Ofa ya Paris St-Germain ya £34.1m kwa ajili ya mlinzi wa Slovakia Milan Skriniar imekataliwa, lakini Inter Milan wanaweza kukubali kuchukua £51.2m kwa ajili ya mlinzi huyo mwenye miaka 27. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Klabu ya Argentina ya River Plate imewasiliana na mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 35 ili ajiunge bure anapomaliza mkataba wake na na klabu hiyo Atletico Madrid msimu huu. (Tuttosport - in Italian)

 

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.