Mfahamu Edward Lowasa, Waziri Mkuu Mstaafu aliyefariki dunia
Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Edward Ngoyai Lowassa {70} amefariki dunia leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar Es Salaam.
Taarifa za kifo chake imetangazwa na Makam wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philip Isdor Mpango
Edward Ngoyai Lowassa anatoka katika ya jamii ya wafugaji Kaskazini mwa Tanzania.
Alizaliwa August 26 mwaka 1953 kijijini Ngarashi Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.
Kitaaluma Lowasa ni msomi , akiwa na shahada kwanza kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam na shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Bath huko Uingereza (1983-1984).
Uzoefu katika siasa
Edward Lowasa ni mtoto wa tatu wa Mzee Ngoyayi.
Ingawa baba yake alikuwa mfugaji aliwahi pia kufanya kazi kama tarishi katika serikali ya wakoloni.
Je Lowassa huyu wa sasa amewahi kuwa nani katika nyadhifa alizozipitia kiserikali?
Edward Ngoyayi Lowassa amewahi, kuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, Ardhi na Maendeleo ya Makazi pamoja na nafasi nyinginezo.
Lakini pia nafasi za juu alizowahi kuzipata ni pamoja na kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania kuanzia mwaka 2005 mpaka Febuari 7 mwaka 2008, alipolazimika kujiuzulu baada ya madai ya kuhusishwa katika kashfa ya rushwa ya Kampuni ya Richmond, Madai ambayo bwana Lowassa aliyakanusha hadi sasa.
Katika siasa,Lowassa anafahamika kama mtu wenye misimamo mikali,kwa kile anachokiamini mwenyewe kama siasa zinazo ambatana na maamuzi magumu.
Post a Comment