WANAWAKE WILAYANI IRAMBA JITOKEZENI KUGOMBEA KWENYE CHAGUZI ZIJAZO
Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Judith Laizer amewataka Wanawake Wilayani Iramba Mkoani Singida kujitokeza kwa wingi na kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 ili kupata wanawake wengi watakao wakilisha kundi hilo katika ngazi za maamuzi.
Hayo yamejiri Januari 31,2024 kwenye sherehe za Umoja wa wanawake wa Tanzania UWT wilaya ya Iramba yaliyofanyika katika Kata ya Ndago kuelekea kilele cha maadhimisho ya Miaka 47 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Laizer amewataka wanawake ndani ya Wilaya kutambua wana haki ya kugombea na kuchaguliwa hivyo ni vyema wakati ikisubiri kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wanawake wanapaswa kujitokeza kugombea nafasi hizo iwe uenyekiti, udiwani na ubunge kwani chama cha Mapinduzi kimetengeneza misingi imara na wezeshi yenye haki sawa kwa wanawake na wanaume katika kugombea kwa kushuhududia kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti w CCM Taifa ambae ni mwanamke akimtaja shupavu.
"Ni kweli ni mwanawake tuna kila sababu ya kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kwani tuna mifano mingi nchi yetu inaongoza na Mwanamama Mwanamke shupavu Rais Dk Samia Suluhu Hassani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama chetu, Bunge letu linaongozwa na mwanamke Dk Tulia Ackson, Wizara mbalimbali zinaongozwa na wanawake na ukiangalia utendaji wa kazi ni mkubwa sana na hata majimbo yanaongozwa na wanawake wenzetu hivyo sisi wanawake wa Iramba ni wakati wetu sasa tujitokeze kwa wingi kugombea bila kuwa na hofu yoyote” Amesema - Judith Laizer.
Ujumbe wa kuhamasisha wanawake kugombea nafasi za uongozi
Katibu huyo wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Judith Laizer amesema uchaguzi wa serikali za mitaa wanawake watakapo jitokeza kwa wingi wataongeza nguvu kuhakikisha Rais Dk Samia Suluhu Hassan anaendela kusalia madarakani kwani hakuna linaloshindikana wakishikamana kwa Pamoja kufanikisha uchaguzi huo utakaompa ushindi kwa ajili ya kuendelea kuleta maendeleo kama yanavyo shuhudiwa kwa sasa.
Pamoja na hayo katibu huyo amewataa wanawake hao na wanachama wa Chama cha Mapinduzi kwa ujumla kuendelea kujisajili uanachama kwa njia ya kielectronic na kupata kadi na kuachana na kadi za zamani ambapo pia wakati wa sherehe hizo jumla ya wanachama 45 walisajiliwa huku zoezi hili likiendelea
Katika hatua nyingine katibu huyo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa utendaji kazi uliotukuka kwa kusimamia nchi na kuleta maendeleo kwani ni miradi mingi imetekelezwa katika kipindi cha uongozi wake ambapo katika sekta mbalimbali Elimu, Afya, Miundombinu n.k huku akiendelea kuteua na kuwaamini wanawake kusimamia nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya serikali na chama
Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Wilaya ya Iramba Judith Laizer akiwa na Katibu wa UWT mkoa wa Singida Ndg Mwasiti Ituja wakiwa na wanawake wengine wakishuhudia bidhaa mbalimbali zinazozaliwa na wanawake hao
Sherehe hizo zimehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT ngazi ya Mkoa na Wilaya ambapo Mgeni rasmi Ali kuwa Katibu wa Umoja huo Mkoa wa Singida Ndg Mwasiti Ituja, Mjumbe wa baraza kuu Mkoa wa Singida Ndg Grace Mkoma, na Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji Mkoa Verian Masangya ambapo michezo mbalimbali ilishuhudiwa kama vile Kukimbiza kuku, kuvuta kamba, kukimbia ndani ya gunia,na kuimba kwaya Pamoja na kukata keki ya miaka 47 ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM.
PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA SHEREHE ZA UMOJA WA WANAWAKE WA TANZANIA UWT WILAYA YA IRAMBA YALIYOFANYIKA KATIKA KATA YA NDAGO KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 47 YA KUZALIWA CHAMA CHA MAPINDUZI.
Katibu wa UWT mkoa wa Singida Ndg Mwasiti Ituja akiwa ameshika bidhaa za wanawake wajasiriamaliKatibu wa UWT mkoa wa Singida Ndg Mwasiti Ituja akisoma jumbe mbalimbali
.
Post a Comment