Tangaza Nasi

UEFA kutoa tuzo tano Agosti

Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) limetangaza kuanza kutolewa kwa tuzo tano mpya za wachezaji bora wa mwaka kuanzia Agosti hii ambazo washindi wake watapatikana toka kura za makocha na wanahabari.

Tuzo hizo zitakabidhiwa huko Monaco nchini Ufaransa hapo Agosti 24 wakati wa droo ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Tuzo hizo 5 mpya ni kwa wachezaji waliofanya vyema kwenye mashindano ya klabu ya UEFA kwa msimu uliopita, kwa mwaka 2016/17,na zitatolewa sambamba na za mchezaji bora wa mwaka kwa wanaume na na wanawake.

Jiunge na BongoTune sasa 

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,  na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo Tune

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.