Watano Kusajiliwa Stamford Bridge
Wakati taarifa za kuondoka kwa mshambuliaji kutoka nchini
Hispania Diego Costa zikiendelea kushika kasi katika vyombo vya habari
nchini Engalnd, meneja wa mabingwa wa soka nchini humo Chelsea Antonio
Conte, ameendelea kusisitiza usajili wa wachezaji watano watakaoongeza
nguvu katika kikosi chake.
Gazeti la The Mirror limeeleza kuwa, Antonio Conte amedhamiria kufanya usajili wa wachezaji wenye uwezo mkubwa kisoka, na tayari ameanza na mpango wa kutaka kumrudisha mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Romelu Lukaku akitokea Everton.
Usajili wa mshambuliaji huyo unatajwa kufikia Puni milioni 70 ambazo zinahitajika huko Goodson Park yalipo makao makuu ya klabu ya Everton.
Wengine wanaopendekezwa na Antonio Conte ni Leonardo Bonucci na Alex Sandro kutoka Juventus, Tiemoue Bakayoko (AS Monaco) na Marco Verratti (PSG).
Katika hatua nyingine kuna uwezekano mkubwa wa Antonio Conte akawaacha Nemanja Matic na Cesc Fabregas.

Post a Comment