CCM wahofia kuchukua fomu Kibiti
Wakati hali ya wasiwasi ikizidi kushamiri kwa wakazi wa wilaya za Kibiti
na Rufiji juu ya usalama wa maisha yao kutokana na kuendelea kwa
matukio ya mauaji, hofu hiyo bado imetanda miongoni mwa wanachama wa CCM
wanaohofia kuchukua fomu za kuwania uongozi ngazi ya matawi na shina.
Akizungumza na gazeti la Mwananchi kwa njia ya simu ,
Katibu wa Siasa na Uenezi wa chama hicho katika wilaya hizo, Mussa
Mnyeresa amesema sababu za wanachama kususa kuchukua fomu hizo hasa
ngazi za tawi, shina na nafasi nyingine ni mfululizo wa matukio ya
mauaji yanayoendelea katika wilaya hizi.
Amesema katika wilaya ya Kibiti, kata za Mjawa, Ruaruke na Mchukwi
yanaongoza kwa wanachama wa chama hicho kutochukua fomu za kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi.
Aidha amesema katika wilaya ya Rufiji uchukuaji fomu za nafasi za
uongozi Tarafa ya Ikwiriri yenye Kata tatu za Umwe, Mgomba na Ikwiriri
napo zoezi la uchukuaji fomu wa nafasi hizo si la kuridhisha.
Mnyeresa amesema hadi sasa kasi ya uchukuaji fomu hizo katika kata
hizo bado ipo chini huku viongozi wa chama hicho wakiendelea
kuwahamasisha wanachama wa chama hicho wachukue fomu.


Post a Comment