Wanaochochea siasa kupitia Whatsapp nchini Kenya waonywa
Tume ya uwiano na utengamano wa kitaifa nchini Kenya inasema inachunguza makundi 21 ya Whatsapp yanayosambaza ujumbe wa chuki na uchochezi kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi ujao.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Francis
Ole Kaparo amesema, tayari wameanza mchakato wa kuwahoji wamiliki wa
makundi hayo ya Whatsapp kutoka kaunti 21.
Kaparo amesema Tume yake itawafungulia mashtaka wale wote
wanaochochea au kutuma ujumbe wa chuki kwa lengo la kuzua machafuko
kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika tarehe nane.
Wakati uo huo, Tume ya Mawasiliano nchini humo imevitaka vyombo vya
Habari nchini humo kutotangaza matokeo ya urais kabla ya Tume ya
Uchaguzi kufanya hivyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Francis Wangusi amesema Tume hiyo
inafahamu kuwa kuna vyombo vya Habari ambavyo vitakuwa vinajumuisha
matokeo ya urais, na kuvitaka kutangaza matokeo yake baada ya IEBC
kufanya hivyo.
Aidha, amesema kuwa Tume hiyo haina nia ya kufunga mitandao ya
kijamii kama facebook,Twitter, Whatsapp na mitandao mingine ya kijamii
kipindi chote cha Uchaguzi Mkuu.


Post a Comment